Nenda kwa yaliyomo

David Raum

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
David Raum

David Raum (hutamkwa kwa Kijerumani: Daavid Raoum; aliyezaliwa 22 Aprili 1998) ni mchezaji wa kulipwa wa mpira wa miguu wa Ujerumani anayocheza katika nafasi ya kiungo wa kushoto au beki wa kushoto.

Anachezea klabu ya RB Leipzig ya Bundesliga, ambako pia ni nahodha wa timu, pamoja na timu ya taifa ya Ujerumani.

Maisha ya Klabu

[hariri | hariri chanzo]

Greuther Fürth

[hariri | hariri chanzo]

Raum alizaliwa Nuremberg, Ujerumani, na alianza kucheza mpira wa miguu katika klabu ya eneo hilo ya Tuspo Nürnberg akiwa na umri wa miaka minne.

Akiwa na umri wa miaka minane, aligunduliwa na kujiunga na akademi ya vijana ya SpVgg Greuther Fürth, iliyokuwa katika mji jirani. Aliendelea kupitia ngazi mbalimbali za timu za vijana za klabu hiyo.

Akiwa mchezaji wa chini ya miaka 19, Raum alianza kupata uzoefu katika timu za wakubwa na akawa sehemu ya kikosi cha kwanza kuanzia msimu wa 2017–18 wa 2. Bundesliga.[1][2]

  1. ↑ https://datencenter.dfb.de/en/data-center/people/david-raum/player
  2. ↑ https://www.worldfootball.net/person/pe350658/david-raum/
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu David Raum kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.