Julian Alvarez
Álvarez akiwa na Argentina katika Kombe la Dunia 2026 | |||
| Taarifa binafsi | |||
|---|---|---|---|
| Jina kamili | Julián Álvarez | ||
| Tarehe ya kuzaliwa | 31 Januari 2000 | ||
| Mahali pa kuzaliwa | Calchín, Argentina | ||
| Kimo | 1.70 m (5 ft 7 in) | ||
| Nafasi anayocheza | Mshambuliaji | ||
| Taarifa za klabu | |||
| Klabu ya sasa | Atlético Madrid | ||
| Namba | 19 | ||
| Kazi katika klabu | |||
| Miaka | Timu | Mechi† | (Goli)† |
| 2018–2022 | River Plate | 74 | (34) |
| 2022–2024 | Manchester City | 67 | (20) |
| Timu ya Taifa ‡ | |||
| 2018–2019 | Argentina U20 | 15 | (2) |
| 2019–2021 | Argentina U23 | 9 | (2) |
| 2024 | Argentina Olimpiki | 4 | (0) |
| 2021– | Argentina | 60 | (15) |
| 2024– | Atlético Madrid | 69 | (25) |
| * Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 23 Septemba 2026. † Appearances (Goals). | |||
Julian Alvarez (alizaliwa 31 Januari 2000) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka nchini Argentina anayecheza nafasi ya mshambuliaji katika klabu ya Atletico Madrid inayoshiriki Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) na timu ya taifa ya Argentina. Anachukuliwa kuwa mmoja wa washambuliaji bora zaidi duniani.[1]
Alvarez alianza kazi yake ya soka nchini Argentina katika chuo cha vijana cha River Plate, ambapo alicheza mechi yake ya kwanza katika timu ya wakubwa mwaka 2018. Alidumu klabuni hapo kwa misimu minne na kutwaa Kombe la Argentina linaloandaliwa na shirikisho la nchi hiyo, kombe la klabu bingwa barani amerika kusini, na Ligi Kuu ya Argentina mwaka 2021 akiwa mfungaji bora wa mashindano hayo, kisha akachaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Amerika Kusini. Mwaka 2022 alijiunga na Manchester City, ambapo alishinda mataji matatu makubwa kwa msimu mmoja Ligi Kuu ya Uingereza, Kombe la FA, na ligi mabingwa ya ulaya katika msimu wake wa kwanza, kabla ya kuhamia Atletico Madrid mwaka 2024 kwa ada iliyoweka rekodi ya klabu hiyo ya karibu euro milioni 95.
Katika ngazi ya kimataifa, Alvarez aliiwakilisha Argentina katika timu za vijana kabla ya kucheza mechi yake ya kwanza katika timu ya wakubwa mwaka 2021. Alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa ubingwa wa Copa Amerika mwaka 2021, Finalissima 2022 ambapo hukutanisha bingwa wa ulaya na bingwa wa Amerika kusini, Kombe la Dunia la FIFA 2022, Copa Amerika 2024, na kufika fainali ya Kombe la Dunia la FIFA 2026.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Ranked! The 20 best strikers in the world" (kwa English). FourFourTwo. Iliwekwa mnamo 22 Septemba 2026.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link)
| Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Julian Alvarez kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |